Jumatano 18 Novemba 2026 - 07:30
Ujumbe wa rambirambi wa Ayatullah Al-Udhma Sistani kufuatia kufariki kwa Ayatullah Wahid Khorasani

Hawza/ Ayatullah Sistani ametoa ujumbe wa rambirambi kufuatia kufariki Ayatullah Wahid Khorasani, mmoja wa Maraji' wa Taqalidi.

Kwa mujibu wa taarifa ya Idara ya Kimataifa ya Shirika la Habari la Hawza, Ayatullah Sayyid Ali Sistani ametoa ujumbe wa rambirambi kufuatia kufariki Ayatullah Al-Udhma Hussein Wahid Khorasani, mmoja wa Maraji' wa Taqalidi.

Katika ujumbe huo, Ayatullah Sistani ameeleza huzuni na masikitiko yake makubwa kutokana na kufariki Ayatullah Wahid Khorasani, huku akiitukuza nafasi na hadhi ya juu ya Maraji' huyo katika kutetea Uimamu na Wilaya ya Ahlul-Bayt wa Mtume (amani iwe juu yao).

Aidha, akizungumzia juhudi za kipekee za Ayatullah Wahid Khorasani katika nyanja za ufundishaji na malezi, utoaji wa mawaidha na kuwaongoza watu, amesisitiza kuwa huduma zake za kielimu na kidini zitaendelea kubaki katika kumbukumbu za watu daima.

Vilevile, Ayatullah Sistani amemuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu, kwa heshima ya huduma alizozitoa mwanachuoni huyo mashuhuri kwa elimu na watu wa elimu, amjaalie daraja za juu kabisa Peponi na amkusanye pamoja na Mtume Mtukufu Muhammad (s.a.w.w.) na kizazi chake kitakasifu.

Mwisho wa ujumbe wake, Maraji' huyo ametoa rambirambi zake kwa msiba huu mkubwa kwa Mtukufu Wali Al-Asr (Mwenyezi Mungu aharakishe kudhihiri kwake), Hawza za kielimu, familia na wapenzi wa Ayatullah Wahid Khorasani, hususan wanawe, pamoja na waumini wote kwa jumla. Aidha, amewaombea wafiwa wawe na subira njema na kupata malipo makubwa kutoka kwa Mwenyezi Mungu.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha